Rais Magufuli Atuma Salamu za Pongezi Kwa Kenyatta

Rais John Magufuli amemtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo kwa mhula wa pili.
Rais Magufuli ametuma pongezi hizo leo Jumamosi kupitia ukurasa wake wa twitter ‘Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema’ ameandika Rais Magufuli.

magufuli
Matokeo ya urais yalitangazwa jana saa nne usiku ambapo Rais Kenyatta alipata kura 8, 203,290 sawa na asilimia  54.27 huku Raila Odinga aliyegombea kwa mwamvuli wa muungano wa Nasa akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 6, 762,224 sawa na asilimia 44.74.
Hata hivyo, marais wengine wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) walituma salamu zao za pongezi muda mfupi baada ya matokeo hayo kutangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati.
Wakauu hao wa EAC waliotuma salamu zao za pongezi kupitia kurasa zao za twitter ni pamoja na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye amechaguliwa hivi karibuni kuongoza nchi hiyo kwa mhula wa tatu.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s